Kituo cha habari cha jarida la Ufaransa Le Nouvel Observateur kimeandika kuwa katika mazungumzo hayo binafsi Sarkozy alimwambia Obama kwamba hawezi kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu na kwamba ni mtu mrongo na kidhabi. Obama alimjibu kwa kusema kwamba naye pia analazimika kumstahamili Netanyahu kila siku. Habari hiyo imefichuliwa na kituo cha habari cha Arret sur inages.
Wakati wa mazungumzo hayo yaliyofanyika kandokando ya mkutano wa kundi la G20 nchini Ufaransa, vipokea sauti vinavyowekwa masikioni (headphones) vinavyotarjumu lugha mbalimbali vilifunguliwa mapema na kutolewa kwa wandishi habari na baadhi ya waandishi hao waliokuwa tayari waweviweka masikio walisikia mazungumzo hayo ya Sarkozy na Obama.
Mtandano wa Arret sur inages umesema kuwa katika mazungumzo hayo Barack Obama alimlaumu Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kutokana na hatua ya Ufaransa ya kupigia kura ya ndiyo suala la Palestina kupewa uanachama kamili katika shirika la UNESCO na akasema hakutarajia kwamba Ufaransa ingechukua msimamo kama huo!
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 277385
Katika mazungumzo yao binafsi yaliyonaswa na waandishi habari bila ya wao kujua, viongozi wa Ufaransa na Marekani Nicolas Sarkozy na Barack Obama walimtaja Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamini Netanyahu kuwa ni mtu mrongo na kidhabi ambaye hawezi kustahamilika.